+255 786 200 518 info@ohide.or.tz

JISAJILI KUSHIRIKI MAFUNZO YA UONGOZI 2019 NA OHIDE TANZANIA

TANGAZO LA MAFUNZO KWA VIONGOZI WA ASASI ZA KIRAIA

Asasi ya Kiraia ya OHIDE Tanzania yenye makao makuu wilayani Kasulu Mkoani Kigoma, inawatangazia viongozi wa asasi za kiraia na vikundi vya kijamii kuwa watatoa udhamini wa kushiriki mafunzo ya Uongozi, Mawasiliano ya Jamii, Utatuzi wa Migogoro pamoja na utunishaji wa mifuko ya fedha za vikundi au mashirika yao.

Mafunzo hayo ya kimataifa yatafanyika Mjini Kasulu mkoani Kigoma kuanzia Tarehe 29/07/2019 hadi 02/08/2019, na wakufunzi watatoka katika taasisi iliyobeboa kwa ufundishaji wa uongozi na utafutaji wa pesa kutoka nchini Uholanzi. shirika hilo linaitwa Libre Foundation na litawagharimiwa waalimu watakaokuja Kasulu kutoa mafunzo hayo.

Kwa kuwa elimu ni gharama na mashirika mengi hayana uwezo wa kugharimia viongozi wao kwenda kusoma masuala ya uongozi na utatuzi wa migogoro, OHIDE imeandaa udhamini kwa viongozi 15 tu kushiriki mafunzo hayo bila malipo.

Gharama ya mafunzo kwa kila siku ni sh 20,000/= hivyo washiriki ambaoo hawatapata udhamini huo na wanapenda kusoma kwa wiki moja itabidi walipie sh. 100,000.

Namna ya kuomba ni kujaza fomu maalumu inayopatikana katika tovuti ya OHIDE ambayo ni www.ohide.or.tz au piga simu namba zifuatazo upate maelekezo. 0786200518 au 0754041224 ili upewe maelekezo, au fika ofisi zetu zilizopo Mwilamvya jirani na halmashauri ya Mji wa Kasulu.

Karibu ujiimarishe kiuongozi ili ulisaidie shirika lako, usikubali kukosa ofa hii, Veti vinavyotambulika kimataifa vitatolewa kwa washiriki wote. Mwisho wa maombi ni tarehe 13/05/2019 Siku ya JUMATATU SAA SABA MCHANA.

BOFYA AU BONYEZA HAPA UPATE FOMU YA KUJISAJIRI BURE

Kama unahitaji maelekezo ya namna ya kuijaza fomu hii, tafadhali wasiliana nasi ili upate maelekezo sahihi. Namba zetu ni 0754041224 au 0764243377

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Captcha loading...