+255 786 200 518 info@ohide.or.tz
WhatsApp Image 2017 09 03 At 10.45.03 AM

Mafunzo ya Uongozi na mawasiliano kwa Asasi za kiraia

Mratibu wa Mafunzo mkazi wa Libre Foundation Ndg Prosper Kwigize akikabidhiwa cheti cha kuhitimu mafunzo ya Uongozi katika hafla iliyofanyika katika fukwe za Ziwa Victoria mjini Bukoba 2016

Shirika letu linapenda kuwajulisha kuwa, Mafunzo ya Uongozi na Mawasiliano kwa Viongozi wa Asasi za kiraia (NGO, CBO, LBO na CSO) Yatafanyika wilayani Kasulu Mkoani Kigoma tarehe 22-26 October 2018.

Muda wa maombi ya kushirikii umeshamalizika na waliowasilisha fomu zao zinafanyiwa uchambuzi na watakaoteuliwa kushiriki mafunzo watataarifiwa mapema ili wajiandae kushiriki mafunzo hayo muhimu ya siku tano ya Kimataifa.

Waandaaji wa mafunzo hayo ni shirikala OHIDE Tanzania lenye makao makuu yake wilayani Kasulu, Wakufunzi ni wataalamu wa uongozi na mawasiliano kutoka shirika la kimataifa la Libre foundation la Uholanzi na mratibu mkazi wa mradi namba 143 wa mafunzo nchini Tanzania ni ndugu Prosper Kwigize.

Tunataarifu Umma kuwa hatupokei tena maombi kwa ajili ya mafunzo hayo. tunakaribisha maoni na maswali kwa anuani zetu zilizopo katika mtandao huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Captcha loading...