+255 786 200 518 info@ohide.or.tz
WhatsApp Image 2017 09 03 At 10.25.49 AM (1)

Nafasi za Mafunzo ya Uongozi na Utunishaji wa mfuko kwa NGO Tanzania- MPYA 2019

Shirika lisilo la Kiserikali la OHIDE Tanzania kwa kushirikiana na shirika la kimataifa linalotoa mafunzo kwa mashirika ya kiraia duniani la Libre Foundation, wanakutangazia fursa ya mafunzo kwa viongozi wa asasi za kiraia nchini Tanzania awamu ya pili mkoani Kigoma.

Mafunzo haya yanakuja kufuatia kumalizika kwa mafunzo kama hayo mwaka jana ambapo viongozi wengi walikosa fursa hiyo na kuomba yarejewe tena ili wengine wapate fursa hiyo Adimu.

Mafunzo yatafanyika mwezi wa Nane (August 2019) mjini Kasulu. Aidha mafunzo haya kwa kawaida hupaswa kulipiwa kiasi cha sh. 100000 kwa siku TANO sawa na EUR 8 kwa siku. Hata hivyo OHIDE kwa ktambua umhimu wa mafunzo na uwezo wa asasi nyingi, imetoa udhamini kwa washiriki kumi na tatu (15) ambao watahudhuria mafunzo hayo BURE KABISA.

Kikosi cha Viongozi 16 wa mashirika mbalimbali kutoka Kasulu, Kigoma na Babati kilifurahia kupata vyeti vya kimataifa vya kuhitimu mafunzo ya uongozi na mawasiliano. Bado zamu yako.

SIFA ZA MSHIRIKI
1. Awe kiongozi kutoka asasi au shirika la kiraia
2. Awe anawakilisha shirika ambalo uwezo wake wa kiuchumi ni wa Bajeti ya chini ya EUR 100,000 kwa mwaka
3. Awe anajua kusoma, kuandika na kuongea Kiingereza
4. Awe amejiandaa kuhudhuria mafunzoni siku tano bila kukosa

MASOMO YATAKAYOFUNDISHWA

1. Uongozi (Leadership and governance)
2. utunishaji wa mfuko wa shirika (Fundraising)
3. Mawasiliano (Social communication)
4. Utatuzi wa Migogoro (Conflict resolution)

NAMNA YA KUOMBA UDHAMINI

Ili kiongozi wa asasi apate fursa ya kushiriki mafunzo haya kwa kulipiwa gharama na OHIDE Tanzania anapaswa kuwahi pamema kutuma maombi yake ya kushiriki mafunzo na kupata udhamini. maombi yatumwe kwa

Katibu Mtendaji
OHIDE Tanzania
SLP 490 Kasulu, Kigoma
Barua Pepe: info@ohide.or.tz

Au fika katika ofisi zetu zilizoko kasuluu Mjini jirani na halmashauri ya Mji mtaa wa Mwilamvya jirani na kituo cha mafuta barabara ya kwenda Soko la Mwilamvya.

WAHI UPATE UDHAMINI, KUMBUKA ELIMU NI GHARAMA

KARIBUNI TUELIMISHANE

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Captcha loading...