+255 786 200 518 info@ohide.or.tz
Baldoyle Training 720×480

Tangazo la nafasi za mafunzo

Asasi ya OHIDE Tanzania yenye makao makuu katika Halmashauri ya Mji wa Kasulu mkoani Kigoma
kwa kushirikiana na shirika la kimataifa la Libre Foundation la nchini Uholanzi tutatoa mafunzo ya
uongozi kwa asasi za kiraia mkoani Kigoma hivi karibuni.
OHIDE Inatambua kuwa vikundi vingi vya kijamii pamoja na asasi za kiraia zinakosa maendeleo na
kushindwa kutimiza ndoto zake kutokana na ombwe la ujuzi mdogo wa masuala ya uongozi na utawala
wa watu na mali, kwa kutambua hilo OHIDE inawaalika viongozi wa asasi (NGOs) wenye nia ya
kuongeza ujuzi katika kusimamia asasi zao walete maombi mapema kwa anuani ifuatayo:-
Katibu Mkuu;
Organization for Human Investment and Development (OHIDE Tanzania)
P. O. Box 124
Kasulu, Kigoma
Email: ohidetz@gmail.com
Website: www.ohide.or.tz
Mafunzo yataendeshwa na wakufunzi waliobobea kutoka Nchi za Umoja wa Ulaya wakishirikiana na
wataalam wa ndani ya nchi na yataendeshwa kwa vitendo ili kumpa mshiriki ujuzi wa kutosha wa
kusimamia ASASI (NGO)
Mafunzo hayo yatafanyika kwa siku tano katika mfumo wa master class kuanzia tarehe 22-26 October
2018 mjini Kasulu mkoani Kigoma. Kumbuka wahitaji wa mafunzo ya uongozi na utawala ni wengi hivyo
ni busara sana kutuma maombi mapema ili uletewe fomu ya ushiriki na maelekezo
Nafasi ziko wazi kwa asasi zote za kiraia za mkoani Kigoma.
Ili kuifahamu Ohide Tanzania tafadhali tembelea kurasa zetu katika mitandao ya kijamii pamoja na
website yetu ya www.ohide.or.tz. Kwa mawasiliano zaidi unaweza kupiga simu 0786200518, 0754041224.

Bonyeza Hapa Kupakua fomu ya kujiunga na mafunzo

This Post Has 2 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Captcha loading...